Mkimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour amewataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni kusimamia na kutunza kwa karibu miundombinu iliyopo .
Amezungumza hayo wakati alipokuwa anatembelea na kuzindua miradi ya Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Handeni tarehe 28/9/2017,amesema kuwa Serikali inatumi fedha nyingi, Wananchi wamejitolea kuchangia gharama kubwa hivyo kuharibika kwa miundombinu hiyo ni sawa na kutoitendea haki Serikali na nguvu kubwa Wananchi waliojitolea kuchangia kwenye miradi ya maendeleo.
Ndg.Amour amesema kuwa ili kutekeleza uchumi wa viwanda nchini kwetu tunahitaji wasomi wanasayansi, wakulima bora kwa kuzingatia utunzaji bora wa mazao yetu na kuongezea thamani bidhaa zetu, Afya zilizoimarika kwa wananchi wote, viwanda vidogovidogo na kwamba hakuna budi kuhakikisha miundombinu inatunzwa na kuimrisha afya zetu.
Amepongeza pia Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa namna ambavyo imetekeleza maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kufungua Bohari ndogo ya Dawa na ujenzi wa Maabara bora za kisayansi kwa shule za Sekondari zitakazowezesha kuwa nawahitimu wazuri wa Sayansi ili kufikia malengo ya kuwa Tanzania yenye uchumi wa Viwanda.
Alipokuwa anazindua Bohario ndogo ya Dawa Ndg. Amour ametoa rai kwa wananchi kuacha kutumia dawa kama chakula bila kufuata taratibu za vipimo na ushauri kutoka kwa madaktari na kwamba wanapohisi dalili za kuumwa wafike Hospitali kupata maekezo juu ya matumizi sahihi ya dawa husika.
Aidha Amewataka wananchi kuondoa dhana kwamba dawa zinazotengenezwa nje ya Nchi ni bora zaidi kuliko zile zinazotengenezwa Tanzania huku akitolea mfano wa dawa aina ya panadol inayotengenezwa nchini Kenya.
Amewatak wafanyakazi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi wote bila kujali tofauti na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuendelea kulijenga Taifa letu kwa kupiga vita Rushwa, magonjwa ya Ukimwi na Malaria, Dawa za kulevya na kutoa elimu thabiti kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kuchangia shughuli za kimaendelo kwenye maeneo yao.
Amour amepongeza miradi yote na kutuma salamu za pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ambaye alikuwa na majukumu mengine na nafasi yake kukaimiwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Eng. Robert Gabriel kwa namna ambavyo amejipanga kuhakikisha maendeleo yanapatikana Wilayani Handeni na juhudi kubwa anazofanya.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Robert Gabriel ameahidi kufikisha salamu hizo za pongezi na kuhakikisha maelekezo yote yaliyotolewa na Mkimbiza mwenge Kitaifa Ndg.Amour Hamad Amour yanafanyiwa kazi kwa ukamilifu wake.
Mwaka 2017 Mwenge wa Uhuru umepokelewa na kukimbizwa kwa kilomita 128 katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na umepitia Miradi ya Maendeleo 8 yenye thamani ya Tshs 2,030,619,096/= katika sekta za Elimu, Afya, Kilimo, Maji na Ujasiriamali. Halmashauri imechangia Tsh.106,366,735/=, Serikali Kuu Tsh.568,412,342/=, Nguvu za wananchi Tsh.383,745,607 na wadau wa maendeleo Tsh. 972,094,412/= Kati ya Miradi hiyo 5 imezinduliwa, 2 imewekewa mawe ya msingi, 1 umetembelewa na kukabidhiwa cheti cha utambulisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imekimbiza Mwenge wa Uhuru kuanzia tarehe 28-29/9/2017 na kuukabidhi Wilayani Pangani Mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya MJI Handeni Kenneth Haule akiwa tayari kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe tayari kuukimbiza
Ufunguzi wa Bohari ndogo ya kuhifadhia Dawa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa tayari kuonesha vifaa vinavyotumika kwenye maabara
Muonekano wa nje wa Maabara ya Sayansi Shule ya Sekondari Kwaluguru.
Muonekano wa ndani wa Ghala
Ufunguzi wa Ghala la Kuhifadhia mazao lililopo Kwachaga.
Wataalamu wa Afya na Madaktari wakiwa kwenye chumba cha upasuaji kituo cha Afya Mkata kuonesha wapo tayari kufanya kazi.
Baadhi ya vifaa vilivyopo kwenye jengo la Upasuaji kituo cha Afya Mkata
Mkimbiza Mwenge wa uhuru kktikati akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Handeni Eng Robert Gabriel Kulia na Mratibu wa Mwenge Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Kushoto Mbazi mfinanga na wataalamu wengine mara baada ya kuweka jiwe la Msingi mradi wa tanki la kuhifadhia maji Kijiji cha Kwedikabu Kwamsisi.
Jengo la Kituo cha Afya Kwamsisi lililowekewa Jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru
Mkurugenzi Mtendaji William Mkaufwe kikagua Gwaride la Halaiki
Watumishi na Watalaam mbalimbali wakiwa tayari kuupokea mwenge wa Uhuru eneo la Viwanja vya Mkesha Kwamsisi
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Ndg.Amour Hamad Amour akikagua vifaa vya kufugia samaki vilivyotolewa kwa vikundi vya kinamama na Vijana kama Mkopo badala ya kutoa fedha Taslim.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa