Shirika la kiraia la Hope 4 young girls (Tumaini kwa watoto wa kike) ambayo makao makuu yake yako Dar es Saam lakabidhi vifaa mbalimbali vya kujikinga na ugonjwa hatari wa Korona (COVID 19) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni vyenye thamani ya shilingi milioni tisa (9,000,000) ambapo zoezi lilifanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 11-14/05/2020 katika ya Kata za Kwaluguru, Kwankonje, Kang’ata, Mazingara,Mkata, Misima, Sindeni , Kwamatuku na Makao makuu ya Halmashauri. Vifaa hivyo ni pamoja na ndoo za kuwekea maji 150, sabuni za maji boksi 5, vitakasa mikono boksi 7, mabango yanayotoa elimu kuhusu ugonjwa wa Korona (COVID19) 30 na kinga (gloves) boksi 20.
Akipokea vifaa hivyo Bi. Fatuma Kalovya kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni amewashukuru shirika hilo kwa kumuunga mkono Mh. Rais kwenye juhudi za kupambana na korona (COVID 19) na kwa kuichagua Handeni kuja kutoa msaada huo wa vifaa na kuwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitaenda kutumika vizuri na wananchi kwani wanauhitaji mkubwa wa vifaa hivyo ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo.
Bi Fatuma Kalovya Ametoa wito kwa wadau kuwa pamoja na Kata walizolenga kugawa vifaa hivyo pia wazikumbuke Kata za Kabuku na Segera kwa kuwa ziko barabara kuu na zina mwingiliano mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Hope 4 young girls(Tumaini kwa watoto wa kike) Bi. Salama Kikudo amesema kuwa wao ni wadau wa kutetea haki za watoto wa kike na kutoa elimu dhidi ya mimba za utotoni lakini wameamua kuja kutoa vifaa vya kujikinga na ugonjwa hatari wa Korona (COVID19).
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa