Shirika la kiraia la Hope 4 young girls (Tumaini kwa watoto wa kike) ambayo makao makuu yake yako Dar es Saam lakabidhi vifaa mbalimbali vya kujikinga na ugonjwa hatari wa Korona (COVID 19) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni vyenye thamani ya shilingi milioni tisa (9,000,000) ambapo zoezi lilifanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 11-14/05/2020 katika Kata za Kwaluguru, Kwankonje, Kang’ata, Mazingara,Mkata, Misima, Sindeni, Kwamatuku na Makao makuu ya Halmashauri. Vifaa hivyo ni pamoja na ndoo za kuwekea maji 150, sabuni za maji boksi 5, vitakasa mikono boksi 7, mabango yanayotoa elimu kuhusu ugonjwa wa Korona (COVID19) 30 na kinga (gloves) boksi 20.
Akipokea vifaa hivyo Bi. Fatuma Kalovya kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni amelishukuru shirika hilo kwa kumuunga mkono Mh. Rais kwenye juhudi za kupambana na korona (COVID 19) na kwa kuichagua Handeni kuja kutoa msaada huo wa vifaa na kuwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitakwenda kutumika vizuri na wananchi kwani wanauhitaji mkubwa wa vifaa hivyo ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo.
Bi Fatuma Kalovya alitoa wito kwa wadau kuwa pamoja na Kata walizolenga kugawa vifaa hivyo pia wazikumbuke Kata za Kabuku na Segera kwa kuwa ziko barabara kuu na zina mwingiliano mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Hope 4 young girls(Tumaini kwa watoto wa kike) Bi. Salama Kikudo amesema kuwa wao ni wadau wa kutetea haki za watoto wa kike na kutoa elimu dhidi ya mimba za utotoni lakini wameamua kuja kutoa vifaa vya kujikinga na ugonjwa hatari wa Korona (COVID19).
Wananchi wa Kata zilizopokea msaada huo walishukuru shhirika hilona kuwahakikishia kutumia vifaa hivyo ipasavyo pia wameahidi kutoa elimu kwa watu wengine ili kupambana na ugonjwa hataria wa Korona (COVID 19).
Afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bi. Fatuma Kalovya kulia akiongea baada ya kupokea msaada huo.
Bi. Fatuma Kalovya kulia akipokea sabuni kutoka kwa mwakilishi wa Hope 4 young girls.(Tumaini kwa watoto wa kike).
Afisa maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bi. Rachel Mbelwa akipokea sabuni kutoka kwa mkurugenzi wa Hope 4 young girl(Tumaini kwa watoto wa kike).
Mkurugenzi Mtendaji wa Hope 4 young girls (Tumaini kwa watoto wa kike) kushoto akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo.
Wafanyakazi wa makao makuu ya Halmashauri ya Handeni wakipokea msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Korona(COVID 19).
Mwenyekiti wa Serikeli ya kijiji cha Magamba katikati akiwa na viongozi wa kijiji mara baada ya kupokea msaada wa ndoo za maji, sabuni na vitakasa mikono.
Wananchi wakinawa mikono baada ya kupokea vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa korona kutoka kwa shirika la Hope 4 young girls(Tumaini kwa watoto wa kike)
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa