Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imewapongeza na kuwapa motisha walimu kwa kufaulisha vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika Octoba 2022 ambapo jumla ya wananfunzi 8,896 walifanya Mtihani huo na jumala ya watainiwa 8,620 walisajiliwa na kufanya Mtihani wa Upimaji Kitaifa darasa la nne uliofanyika Mwaka 2022.
Motisha hizo ni pamoja na fedha tasilimu, vyeti vya pongezi kwa walimu waliofanya vizuri pamoja na majiko ya gesi kwa shule zilizo kwenye mazingira magumu ili walimu waweze kuandaa chakula wakiwa ofisini na vyeti vya himizo kwa shule zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe kwenye kikao cha Tathmini ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi na Upimaji Kitaifa darasa la nne uliowakutanisha wadau wa Elimu, madiwani, Wakuu wa Idara, Maafisa Elimu Kata, walimu wakuu wa shule za Msingi zote pamoja na baadhi ya wenyeviti wa vijiji.
Kwenye Kikao hicho Mkuu wa Wilaya Mhe. Mchembe amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kuandaa kikao hicho na kuwapa motisha walimu na amewataka walimu hao kuwa motisha hizo ziwe chachu ya kuongeza zoezi zima la ufundishaji ili ufaulu uongezeke kwa mtihani wa mwaka 2023 uwe wa 100%.
Pia Mhe. Mchembe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya Elimu kwa Wilaya ya Handeni na kuwapatia vishikwambi walimu wote na kuwaelekeza vitumike kama Serikali ilivyolenga ili vilete tija kwenye ufundishaji na ujifunzaji na kufuata kaulimbiu ya Handeni isemayo “kuongeza Kichwa kuondoa mkia” ikiwa na maana kuongeza ufaulu wa alama A na kuaondoa ziro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Stephen ametambua jitihada zilizofanywa na walimu hivyo ameamua kuwapa motisha na jukumu lao ni kufundisha lakini pia wapo baadhi yao wanapenda kukwamisha maendeleo kwa kuchelewa kufika kazini, wanafundisha vipindi vichachache hivyo amemuagiza Afisa Eimu ya Awali na Msingi kuwaangalia kwa jicho la pili walimu wasioendana na kasi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu ili Halmashauri iweze kufikia malengo ya kufanikisha mikakati iliyowekwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Bw. Saitoti ametoa maelekezo kwa walimu kuwa kuhakikisha shule zote za Msingi na Sekondari zinatoa chakula ili kukuongeza hali ya ujifunzaji kwa wanafunzi.
Kwa upande wa walimu waliopokea tuzo hizo walimshukuru na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa motisha na kuahidi matokeo mazuri zaidi mwaka huu 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe, aliyesimama akiongea kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mhe. Mussa Mwanyumbu, aliyesimama akiongea.
Bw. Saitoti Stephen ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni, akitoa maelekezo kwa walimu.
Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Handeni wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya.
Wilimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya.
Baadhi ya Zawadi zilizotolewa na kukabidhiwa kwa walimu.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa