Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Handeni limekubaliana kwa pamoja kuhamasisha wananchi kulima mazao ya biashara ambayo ni Muhogo , korosho, pamba na Katani Ili kuinua uchumi wa Halmashauri.
Makubaliano hayo yamefanyika kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 15-16/2/2018 Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Akizungumza na waheshimiwa Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh.Ramadhani Diliwa alisema kuwa lazima wananchi wahimizwe kulima mazao mbadala sio kung'ang'ania mahindi wakati ardhi ya Handeni inakubali mazao mengine ambayo yataimarisha uchumi wa Jamii nzima.
Aliongeza kuwa Halmashauri imejipanga kuleta mapinduzi hivyo kila mmoja awajibike kwenye eneo lake kuhakikisha malengo yanafikiwa kwani kuna miche 10000 ambayo tayari imeandaliwa na fedha kwaajili ya kununua mbegu nyingine imetengwa tayari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw William Makufwe alisema kuwa Halmashauri inataka walau kwa kuanzia kuwa na ekari 1000 Za zao la korosho ambapo Kata ambazo zitachangamkia fursa zitakuwa za Kwanza kupatiwa mbegu kwani uhakika wa mbegu upo.
Aidha alishauri kwa watu ambao wanauwezo wa kununua mbegu waweze kununua kwani hazina gharama kiasi cha kushindwa kununua ili kuleta mabadiliko na mwitikio mzuri kama ambavyo wananchi walivyoitikia kwenye zao la Muhogo.
Wa Kwanza Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe, katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa akifiatiwa na Makamu Mwenyekiti Mh Abdalla Pendeza
Wataalamu na Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
Waheshimiwa Madiwani
Baraza likiendelea.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa