Wataalamu wa mifugo na mazao wametakiwa kuhakikisha zoezi la utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo linafanyika kwa weredi na kuacha urasimu kwa kufuata sheria na kanuni zinazoongoza utambuzi wa mifugo.
Rai hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi. Upendo Magashi(Afisa Tawala) leo alipokuwa akifungua mafunzo ya wataalamu wa mifugo kuhusu sheria ya utambuzi usajili na ufuatiliaji wa mifugo , uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Handeni.
Amesema kuwa hili ni agizo la kitaifa lenye lengo la kutambua mifugo iliyopo kila eneo ili kubaini idadi ya mifugo na rasilimali zinazohitajika kwenye uendelezaji wa mifugo, amesema Ili kuweza kutambua idadi kamili ya mifugo iliyopo katika wilaya yetu ni lazima kufanya zoezi la utambuzi usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa kuzingatia sheria namba 12 ya mwaka 2010 inayohusu utambuzi,usajili na ufuatiliaji wa mifugo(livestock identification registration na tracebility act 2010) na kanuni zake za mwaka 2011.
Ameongeza kuwa zoezi hili ni shirikishi na wananchi wote wanapaswa kuhamasishwa na kuelimishwa ili kuondokana kabisa na kesi zinazotokana na wakulima na wafugaji waliopo kwenye Wilaya yetu; amesema kwa kufanya utambuzi wa mifugo kutasaidia kupunguza na kuondoa migogoro inayotokana wakulima na wafugaji, kutambua mifugo inayoingia wilayani kwetu kinyume na taratibu, kumwezesha mfugaji kutambua mifugo yake na kurahisisha utambuzi wake pindi mfugo unapopotea.
Aidha amesema kuwa kutokana na sheria ya utambuzi usajili na ufuatiliaji wa mifugo kila mfugo kijijini unatakiwa kutambuliwa kwa kuwekewa chapa ya moto ambayo ni maalumu kwa kila Kijiji.utambulisho huu utasaidia kujua mifugo ambayo ni halali kwa Kijiji husika na ile amabyo ipo kijijini isivyo halali pia litaondoa tatizo la kuhamahama kwa wafugaji.
“ yeyote atakayebainika kuwa kikwazo cha utekelezaji wa zoezi hili taarifa ifikishwe kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuona ni namna gani kamati ya Ulinzi na Usalama itamshughulikia” amesema Upendo.
Ametoa rai kwa wataalamu wa mifugo kuthamini mazao ya wakulima hususani pindi yanapovamiwa na mifugo,amesema kumekuwepo na kesi nyingi za wakulima na wafugaji juu ya uharibifu wa mazao, kila mmoja awajibike kwa nafasi yake kwani uwepo wao kwenye ngazi ya Vijiji na Kata sio wa makosa.
Kwaupande wake kaimu Mkurugenzi Bw. Amani Mangesho(Mwanasheria wa Halmashauri) amewataka watalamu wa mifugo na kilimo kuacha kufanya kazi kwa mazoe na kuendesha zoezi bila ubaguzi na kuangali nani ni nani.
Amewataka wataalamu wa mifugo kusimamia sheri inayowaongoza katika utekelezaji wa zoezi na kuhakikisha mafunzo wanayopatiwa yanawafikia wananchi juu ya umuhimu wa zoezi hili kwa kuzingatia ni agizo la kitaifa na utekelezaji wake unahitajika kwenye maeneo yote.
Baadhi ya Mifugo
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi. Upendo Magashi ( Afisa Tawala) akizungumza na Wataalamu wa Mifugo.
Kaimu Mkuruygenzi Bw. Amani Mangesho ( Mwanasheria wa Halmashauri ) akizungumza na wataalamu wa mifugo)
Baadhi ya Wataalamu wa Mifugo na kilimo
LikeShow More ReactionsCommentShare
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa