Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Handeni limeridhia na kuwapitisha watumishi watano kuwa wakuu wa Idara na Vitengo baada ya kuridhishwa na utendaji wao wa kazi.
Lidhaa hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Ramadhani Diliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya Handeni hivi karibuni.
Diliwa alisema kuwa Baraza lake limetathmini kazi za watumishi hao watano na kuridhishwa na utendaji wao wa kazi na kufikia maamuzi ya kuwapitisha kuwa wakuu wa Idara na Vitengo. Aliwataja watumishi hao na nafasi zao katika mabano kuwa ni Mosses Chilla (Mkuu wa Idara ya Takwimu, Mipango na Ufuatiliaji), Fikeni Senzige (Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi), Julius Omary (Mkuu wa Idara ya Ujenzi na zimamoto), Saturine Kessy (Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani) na Mussa Kimwaga (Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi). Aidha, Napoleone Mlowe aliidhinishwa kuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni alisema kuwa umefika wakati wao kuthibitisha kuwa Baraza la Madiwani halijakosea kuwateu katika nyadhifa hizo kwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa. “Fanyeni kazi kwa weledi kuonesha kuwa Baraza limefanya maamuzi sahihi, pale mnapohitaji ushauri msisite kushirikisha wenzenu” alisema Diliwa.
MOSSES CHILLA (MKUU WA IDARA YA MIPANGO,UCHUMI NA UFUATILIAJI)
FIKENI SENZIGE (MKUU WA IDARA YA ELIMU MSINGI)
JULIUS OMARY (MKUU WA IDARA YA UJENZI)
SATURINE KESSY (MKUU WA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI)
MUSSA KIMWAGA (MKUU WA KITENGO CHA MANUNUZI)
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa