Wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wamepatiwa kadi ya utambulisho wa waze na kuhamasishwa kujiandikisha kwaajili ya kupata kadi hizo ili kuweza kupata huduma ya matibabu bure kwa wazee.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ametoa rai hiyo jana kwenye ofisi ya Kata ya Kamsisis na kuwapa utaratibu wa namna watakavyoweza kupata vitambulisho kwaajili ya utambulisho wao pindi watakapokwenda kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya kwaajili ya matibabu.
Mh. Gondwe alisema kuwa ni dhamira kuu ya Mh. Rais kuona waze wote wenye umri kuanzia miaka 60 wa Tanzania wanapata huduma za matibabu bure na kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imejipanga kuhakikisha wazee wote waliopo kwenye Halmashauri wananfikiwa na kupata huduma za matibabu buree.
“Kadi ya utambulisho wa mzee itakusaidia kupata huduma za afya bure na haraka, wazee wetu ni wa thamani na mmelitumikia taifa hili vyema, ni jukumu letu kuhakikisha mnapata huduma bora za afya, wazee wengine ambao hamjajitokeza kupiga picha mjitokeze ili muweze kupata vitambulisho”Alisema Mkuu wa Wilaya.
Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi Bi.Edna Katailaya aliwataka viongozi wa Vijiji kuhakikisha wanahamasisha wananchi kuchangia ghara za laki mbili kila kijiji kwaajili ya kufidia gharama zao kwenye vituo vya afya kama Uongozi wa Halmashauri ulivyoelekeza awali.
Aidha,kutokana na gharama kubwa za huduma za matibabu Halmashauri ya Wilaya ya Handeni iliweka utaratibu wa kila Kijiji kuchangia gharama za laki mbili (200,000) kwaaajili ya kufidia gharama za matibabu bure kwa wazee kwa kipindi cha mwaka mzima yaani Januari-Desemba kutokana na ufinyu wa bajeti uliopo.
Jumla ya wazee 782 wa Tarafa ya Kwamasisi inayojumisha Kata ya Kwamsisi na Kwasunga wamepatiwa kadi za utambulizho wa wazee,zoezi hilo linaendelea kwenye maeneo yote ya Halmashuri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni kizungumza na wazee wa Kwamsisi.
utoaji wa kadi ukiendelea.
mmoja wa wazee akikabidhiwa kadi na Mkuu wa Wiaya.
mmoja wa wazee akikabidhiwa kadi na Mkuu wa Wilaya.
Kaimu Mkurugenzi Bi.Edna Katalaiya akizungumza na wazee wa Kwamsisi juu ya umuhimu wa vijiji kuchangia fedha ya fidia kwa matibabu ya wazee.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni akizungumza na wazee wa Kwamsisi Faida za kuw na kadi ya utambulisho wa wazee
baadhi ya wazee wa Kwamsisi waliofika kupatiwa kadi zao
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akizungumza na mmoja wa wazee wakati wa uhamasishaji Kata ya Kabuku.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa