Wazee zaidi ya 2000 wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Kata ya Kabuku wamepatiwa kadi ya utambulisho wa wazee kwa awamu ya pili ili kuweza kupata huduma ya matibabu bure kwa wazee.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe ametoa kadi hizo kwa wazee jana wakati akizindua zoezi hilo kwa awamu ya pili na kuwasisitiza wazee kumripoti mtu yeyote atakayeonekana ni kikwazo kwa kupata huduma kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya pamoja na kuwa na kadi ya utambulisho wa wazee.
Amewataka viongozi ngazi ya Tarafa ,Kata na Vijiji kusimamia utoaji wa fedha kiasi cha laki mbili (200,000) zinazotolewa na Serikali za Vijiji kwa mwaka kwaajili ya kuchangia huduma za matibabu bure kwa wazee.
Zoezi la utoaji wa kadi za utambulisho kwa wazee ulianza Novemba 23mwaka2017 ambapo Halmashauri imelenga kutoa kadi hizo kwa wazee 1717 wa Halmashauri ya Wilya ya Handeni.
Baadhi ya wazee wa Kata ya Kabuku waliojitokeza kupokea kadi za utambulisho wa wazee
Mh.Diwani Kata ya Kabuku Amina Mnegero akitoa kadi ya utambulisho wa mzee kwa mmoja wa wazee
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe akizinduz zoezi kwa kutoa kadi ya utambulisho wa wazee kwa mmoja wa wazee.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa