Kijiji cha Msomera kitakuwa ni Kijiji cha mfano kwa ufugaji wa kisasa na wa kibiashara kwahiyo ni lazima tuweke utaratibu wa kufanya lionekane ni eneo la ufugaji wa kisasa.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi mradi maalumu wa makazi ya Kijiji cha Msomera kwa Halmashauri ya Handeni na Kilindi ili kusimamia na kuingiza kwenye bajeti za Halmashuri hizo na kupeleka huduma mbalimbali kwenye eneo hilo la mradi na kuleta maendeleo ya wananchi wa eneo hilo.
Ameziagiza Halmashauri za Handeni na Kilindi zinapoandaa bajeti zao kwa ajili ya mwaka wa fedha ujao zihakikishe zinazingatia mahitaji ya uendelezaji wa huduma kwenye Kijiji cha Msomera ili kuimarisha ustawi wa jamii wa Msomera.
Kijiji cha Msomera kimepokea wananchi waliohama kwa hiari kutoka hifadhi ya Ngorongoro ili kulinda uoto wa asili katika eneo hilo.Mara baada ya Kuwasili kwenye Kijiji hicho wananchi hao walipewa nyumba za kuishi kwenye eneo lenye ukubwa wa hekari 2.5 na eneo la hekari 5 kwa ajili ya kilimo.
Aidha Mhe. Majaliwa amewataka viongozi wanaofanya ziara kwenye Kijiji cha Msomera wahakikishe wanaanzia kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kujitambulisha rasmi ndipo wapatiwe maafisa wa kuongozana nao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni Mhe. Mussa Mwanyumbu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi ya busara aliyofanya ya kuijenga Msomera na kuweka miundombinu ambayo inawasaidia wananchi wa Handeni na ameupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuahidi kuutunza na miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya Handeni inaboreshwa.
Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Albert Msando Mkuu wa Wilaya ya Handeni (Watatu kutoka kulia, mstari wa mbele)
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mhe. Mussa Mwanyumbu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Bw. Saitoti Stephen (Aliyevaa suti nyekundu)
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa