Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba zinazojengwa kwenye kijiji cha Msomela Kata ya Misima kwa ajili ya wakazi watakaohama kwa hiari kutoka kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Mhe. Majaliwa amesema hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inatambulika kama eneo moja wapo la maajabu ya dunia na limeipa heshima kubwa Tanzania na kuipatia Serikali mapato mengi kupitia utalii hivyo lazima ilindwe na kutunzwa kwani ongezeko la watu kwenye hifadhi hiyo linasababisha kupotea kwa maliasili zilizopo kwenye hifadhi hiyo.
Aidha Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameseama kuwa Serikali itahakikisha haki zote za binadamu zinazingatiwa katika zoezi hilo la kuwahamisha wananchi kutoka kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kwenda kwenye maeneo maalum yaliyotengwa kwaajili yao ambayo ni pamoja na makazi yaliyopo kwenye kijiji cha Msomela.
Kwakumalizia Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkao wa Tanga kukutana na viongozi wa vijiji na wananchi wa eneo la mradi huo ili kuendelea kuwaelimisha kuhusu zoezi hilo na umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kutoka kulia) akikagua ujenzi wa nyumba.
Nyumba zinazojengwa kwa ajili ya wananchi wanaohama kutoka kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kumsikiliza Waziri Mkuu katika kijiji cha Msomela.
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Handeni . Haki zote zimehifadhiwa